Serikali za Uganda na Tanzania zasaini Mkataba wa Bomba la Mafuta
Serikali za Uganda na Tanzania leo zimetia saini Mkataba, wa Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Kusainiwa kwa mkataba huu ni hatua muhimu sana kwa Mradi wa EACOP. Unaweka msingi wa mradi huo pamoja na mikataba mingine ya mradi, ikiwa ni pamoja na Mikataba ya Serikali ya Nchi Mwenyeji, Mikataba ya Wabia na Mikataba ya Ufadhili, ambayo sasa itajadiliwa. Mkataba huu unaonyesha uamuzi wa Jamhuri ya Uganda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuanza ujenzi wa bomba la mafuta lenye joto ambalo ni refu zaidi duniani, kwa manufaa ya nchi zote mbili na makampuni ya mafuta lakini pia kwa manufaa ya eneo lote la Afrika Mashariki.
Pia, ni hatua muhimu kwa maendeleo ya Tilenga (mradi wa mafuta wa kaskazini mwa Ziwa Albert) na Miradi mingine ya mafuta ya Kingfisher kwa kuwa bomba la mafuta ni moja ya njia muhimu za kufikia soko kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano (MoU) wa uuzaji wa rasilimali za mafuta na gesi za Ziwa Albert uliosainiwa mwaka 2014 kati ya Serikali ya Uganda na Ushirika wa Makampuni ya Mafuta.
Ushirika wa Makampuni ya Mafuta, CNOOC, Total na Tullow Uganda Operations Pty Ltd zinachukua fursa hii kuzipongeza na kuzishukuru Serikali za Uganda na Tanzania kwa kufikia kwa haraka hatua hii ya kusaini mkataba huu na kwa mchango wao endelevu kwenye utekelezaji wa mradi huu
Washirika wa JV wamedhamiria kikamilifu na wana hamasa ya kutosha ili kufikia lengo la mauzo ya mafuta ya kwanza yaliyopangwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2020 kwa kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali zote mbili ili kuhakikisha kuwa mradi wa EACOP unaendelea zaidi (hususani kukamilisha Mradi wa Mwisho wa Uhandisi, tathmini ya athari ya kimazingira na kijamii na Utafiti wa mwisho wa kiuhandisi wa miamba, udongo na maji) pamoja na maendeleo ya utafutaji mafuta huko Tilenga na Kingfisher.
Leave a Reply