Afya na Usalama

Afya na Usalama

Afya na Usalama ni sehemu muhimu ya mkakati wa Mradi wa EACOP, na moja ya masuala muhimu kwetu. Afya na usalama wa wafanyakazi wetu na wadau ni kipaumbele cha kwanza .

Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) limechukua hatua za kuhakikisha kuwa afya, usalama na masuala ya mazingira yanazingatiwa wakati wote wa kupanga, ujenzi, na hatua za uendeshaji wa shughuli za bomba. Bomba litachimbiwa – na njia itachaguliwa kwa makusudi ili kuepuka hatari ya tetemeko la ardhi, volkano, mafuriko au majanga mengine ya asili.

Mpango wa kudhibiti uvujaji wa mafuta

Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki utakuwa na wajibu wa usalama wa bomba, utafanya kazi kwa kuzingatia kanuni mbali mbali kutoka wakati wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo. Uhandisi na vifaa vinavyotumiwa kama mabomba ni salama na hayatapata kutu au kuvuja. Kabla ya bomba halijapimwa,  maungio yote yatachunguzwa ili kubaini kasoro kwa kutumia mbinu za ultrasonic au radiographic. Wakati wa shughuli za uendeshaji, Kampuni ya Bomba la mafuta itafanya ukaguzi kwa njia ya mtandao kwa kutumia kifaa cha ukaguzi. Ukaguzi wa kwanza utafanyika mapema katika miaka ya mwanzo ya bomba na baada ya vipindi vitavyopangwa baadaye.

Wakati wa tukio dharura kuna valvu kadhaa kwenye bomba lote ambazo zinaweza kuwashwa mara moja kwenye chumba cha udhibiti ili kuzuia mara moja mtiririko wa mafuta kwenye bomba. Pia kutakuwa na hatua za dharura zilizoainishwa vizuri, ambapo rasilimali zinatumwa mara moja ili kupunguza athari za uvujaji wa aina yoyote. Bomba litakaguliwa mara kwa mara ili kubaini na kudhibiti dalili kabla ya kuwa tatizo.

Mara bomba litakapochimbiwa chini na kutumiwa, uhamasishaji wa mara kwa mara wa wadau na ufuatiliaji sahihi utafanyika ili kuzuia uharibifu kwenye bomba unaoweza kufanywa na watu wengine kwa kuchimba bila kujali na shughuli nyingine za ujenzi. Ikiwa bomba limeharibiwa kwa bahati mbaya au hujuma, uvujaji unaweza kubainishwa kwa haraka kwa sababu ya kushuka ghafla kwa msukumo unaorekodiwa. Wakati uvujaji unapohusisha sehemu maalum, mtiririko wa mafuta utasimamishwa haraka iwezekanavyo kwenye vituo vya kusukumia na valvu za kuzuia zitajifunga ili kutenganisha sehemu hiyo na kuzuia uvujaji wowote. Pia kutakuwa na hatua za dharura, ambapo rasilimali zitatumwa mara moja ili kudhibiti na kupunguza athari zozote za uvujaji.

Bomba litafanya kazi saa 24 kwa siku 7 za wiki na litaendeshwa kwa kuzingatia viwango vya juu vya kiufundi na vya. Afya, Usalama, Ulinzi na Mazingila (HSSE).

Takwimu Muhimu

null

1,445km

Bomba la mafuta ghafi

null

216Kbd

kiwango cha mtiririko wa mafuta kwa siku

null

Over 60%

Kuongezeka kwa asilimia ya Uganda na Tanzania wakati wa awamu ya ujenz

null

3.5 Billion

Uwekezaji wa dola bilioni

null

Over 500,000

vifaa kuagizwa kutoka nje