Mazingira

Kujitolea kwenye Ulinzi wa Mazingira

Mradi wa EACOP utahakikisha kwamba masuala ya afya, usalama, kijamii, kiuchumi na mazingira yanashughulikiwa wakati wote wa kipindi cha kupanga, kujenga na uendeshaji wa shughuli za bomba.
Njia litakapopita bomba imechaguliwa ili kukwepa maeneo muhimu ya kimazingira kama vile mbuga za wanyama Maeneo tengefu kama vile hifadhiza misitu na maeneo yenye idadi kubwa ya watu.

Vituo vitawekwa na kuendeshwa kwa umakini  ili kupunguza athari yoyote ya kimazingira na kiikolojia.

Tumeandaa mkataba wa bioanuai ambao unaweka kanuni za kazi yetu. Kwa mujibu wa mkataba huu, tunafanya shughuli zote za EACOP wakati:

TUNAEPUKA athari isiyo ya lazima kwa mazingira, bioanuai na jamii husika.

TUNAPUNGUZA athari yoyote isiyoweza kuepuka kwa mazingira, bioanuai na jamii husika.

TUNARUDISHA katika hali ya awali maeneo yaliyoathirika na kusimamia urejeshwaji wake.

TUNAONDOA athari yoyote ya mabaki ili kupata faida

Tathmini ya athari za kimazingira na kijamii

ESIA: Tathmini ya athari za kimazingira na kijamii ya EACOP
ESIA ni kifupi cha Tathmini ya Kimazingira na Kijamii. Ni mchakato unaobainisha na kutathmini athari za kijamii na ya kimazingira ya Mradi na hatua za kupunguza.

Tathmini ya Kimazingira na Kijamii ya EACOP itafanyika karibu na njia ya bomba la mafuta (kutoka Kabaale – Hoima, Uganda hadi rasi ya Chongoleani, karibu na bandari ya Tanga kaskazini mwa Tanzania) na kituo cha kuhifadhi mafuta pembezoni mwa bahari (huko Chongoleani). Tathmini imefanywa kwa mujibu wa miongozo ya kimataifa, pamoja na sheria za Serikali za Uganda na Tanzania.

Mchakato wa Tathmini ya Kimazingira na Kijamii

Tathmini ya Kimazingira na Kijamii inafanyika wakati mradi unaopendekezwa unaandaliwa. Inapaswa kufanyika kabla mradi haujaanza kutekelezwa.

Mkutano wa mashauriano wa tathmini (Aprili – Mei 2017)

  • Timu za wafanyakazi sasa zinafanya mikutano na taasisi mbalimbali za serikali, serikali za mitaa na wadau wengine na kushirikishana taarifa kuhusu mradi na Tathmini ya Kimazingira na Kijamii
  • Mnaweza kuuliza maswali na kutoa maoni wakati wa mikutano hii
  • Maoni yenu yote yataandikwa na kufanyiwa kazi

Tafiti za kitaalamu :

  • Timu za wafanyakazi zitakuja kijijini kwenu ili kupata taarifa kutoka kwenu kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii yanayohusiana na kujipatia kipato (kilimo, uvuvi, biashara, afya, elimu, utamaduni nk.)
  • Pia zitafanya utafiti kuhusu bioanuai (mimea, wanyama, ubora wa hewa, kelele, utalii)

Mrejesho wa mkutano wa mashauriano

  • Mikutano itaandaliwa kwa ushirikiano na serikali za mitaa, taasisi za serikali na Asasi Zisizo za Kiserikali mara tu mtaalamu anapomaliza kufanya utafiti na tathmini ya athari ili kujadiliana nanyi kuhusu matokeo
  • Hapa tena mtaweza kuuliza maswali na kutoa maoni ambayo yatazingatiwa kwenye ripoti ya Tathmini ya Kimazingira na Kijamii
  • Ripoti hizi zitawasilishwa kwa serikali za Uganda na Tanzania kwa ajili ya kuidhinishwa. Mara tu baada ya kuidhinishwa, mradi unaweza kuendelea. Hatua zote za udhibiti zinazopendekezwa zinapaswa kutekelezwa.

Tathmini zitafanywa na wataalamu kutoka Uingereza (RSK) na wadau nchini Uganda (ECO&PARTNERS) na nchini Tanzania (JSB & COWI)

Takwimu Muhimu

null

1,445km

Bomba la mafuta ghafi

null

216Kbd

kiwango cha mtiririko wa mafuta kwa siku


null

60%

Kuongezeka kwa asilimia ya Uganda na Tanzania wakati wa awamu ya ujenzi

null

3.5 Billion

Uwekezaji wa dola bilioni

null

500,000

vifaa kuagizwa kutoka nje