Marais Museveni na Magufuli waweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi
Marais Museveni na Magufuli waweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi
Rais Yoweri Museveni na mwenzake wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli leo wamezindua ujenzi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki kutoka wilaya ya Hoima, nchini Uganda hadi bandari ya Tanga, nchiniTanzania.
Viongozi hao wawili walitumia fursa hiyo kuthibitisha umuhimu wa utangamano wa haraka wa jumuiya ya Afrika Mashariki ili kurahisha mipango ya pamoja, ufadhili na utekelezaji wa miradi mikubwa ambayo ni muhimu kwa maendeleo na mabadiliko ya ukanda huu.
Bomba la mafuta lenye joto, ambao ni refu zaidi duniani, litagharimu dola bilioni 3.5 na ujenzi wake utakamilika mwaka 2020 ambapo Uganda itajiunga na kundi la nchi zinazozalisha mafuta. Ujenzi wa bomba la mafuta utafanywa na Total E&P, CNOOC na Tullow Oil pamoja na serikali mbili za Uganda na Tanzania. Bomba la mafuta litakapomilika litasafirisha mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa kila siku.
Akizungumza wakati wa sherehe Rais Museveni alimshukuru sana Rais Joseph Pombe Magufuli, serikali ya Tanzania na Watanzania kwa makubaliano mbali mbali na serikali ya Uganda na wabia ambayo yameharakisha mradi huu.
Alisema kwa sababu ya makubaliano mbali mbali na serikali ya Tanzania, gharama ya kusafirisha pipa la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga itakuwa dola 12.2 kwa pipa, na kuyafanya mafuta ya ghafi ya Uganda kuwa na faida hata kwa kiwango cha leo cha dola 50 kwa pipa.
“Kwa niaba ya wananchi wa Uganda ninawashukuru Rais Magufuli na ndugu zetu wa Tanzania kwa makubaliano mbali mbali yanayohusiana na bomba la mafuta. Hakutakuwa na ushuru wa kupitisha mafuta, hakutakuwa na kodi ya ongezeko la thamani, hakutakuwa na kodi ya mapato ya kampuni, wametupa msamaha wa kodi kwa miaka 20, wametupa eneo la bure ambako bomba la mafuta lipita na kuahidi kununua hisa katika bomba la mafuta” alisema Rais Museveni
Rais aliyaomba mataifa yote ya Afrika Mashariki kulichukulia bomba la mafuta la Afrika Mashariki kama mali ya Afrika Mashariki, akibainisha kuwa kwa kugundulika kwa mafuta na gesi katika nchi nyingine katika eneo hilo, bomba litakuwa chombo cha kusafirishia mafuta kuelekea baharini kutoka nchi zote za Afrika Mashariki.
Rais Museveni aliwapongeza wabia katika mradi wa bomba la mafuta (Total, CNOOC na Tullow) na akawahakikishia kuwa kwa na uhusiano mzuri wa kikazi, kila mmoja atafaidika.
Kwa upande wake, Rais Magufuli alimshukuru Rais Museveni na serikali yake kwa kuiamini Tanzania na kuchagua njia ya Tanga kwa mradi licha ya fursa nyingine zilizopo.
Alisema kwa mafuta kuja Tanga, Tanzania sasa itanunua mafuta ghafi kutoka Uganda badala ya kuingia gharama kubwa za kuagiza kutoka nchi za Kiarabu, huku akionyesha kuwa Uganda pia itaiuzia mafutaTanzania kwa gharama nafuu.
Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Tanzania pia itapata ujuzi na utaalamu kutoka kwa wataalamu wa Uganda ambao watakuwa na uzoefu katika sekta ya uchimbaji mafuta.
Aliwahimiza makandarasi ili kuhakikisha kuwa wanakamilisha mradi kwa muda unaotakiwa, akisema kitu chochote kinyume cha hapo kitaleta sifa mbaya kwao na kwa nchi zao.
Leave a Reply