Njia ya Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki
Njia iliyochaguliwa inaanzia Kabaale – Hoima, Uganda na inaeelekea kusini hadi Peninsula ya Chongoleani karibu na bandari yaTanga Tanzania. Njia ya bomba ilichaguliwa na Serikali ya Uganda kwa kuwa ina gharama nafuu zaidi. Bomba hilo litaanzia Hoima, karibu na Ziwa Albert, na kuvuka mpaka wa Uganda na Tanzania kati ya Masaka na Bukoba, karibu na Ziwa Victoria, katika mpaka wake wa magharibi, nchini Tanzania, bomba litapita karibu na Kahama, Singida, Kondoa hadi Tanga. Nchini Uganda, bomba litakuwa na urefu wa kilomita 296. Nchini Tanzania, bomba litakuwa na urefu wa kilomita 1,149 na litapita katika mikoa 8 na wilaya 24.