Awamu ya Ujenzi
Mara Uamuzi wa Mwisho wa Uwekezaji. Utakapokuwa umefanywa, upembuzi yakinifu, manunuzi na ujenzi wa bomba la mafuta utaanza na kukamilika ndani ya miezi 36
Ujenzi utahusisha:
1.Ujenzi wa Bomba la mafuta
Mara litakapokamilka, bomba litafukiwa kwa uangalifu kwenye mfereji uliochimbwa au, wakati mwingine itabidi lipite chini ya maji au barabara
2. Ujenzi wa Vituo vya Muda
Vituo vingine vitajengwa kama vile;
- Maeneo ya Kupaka rangi & kuhifadhia mabomba
- Ujenzi wa eneo la ziada la kufanyia kazi (Mafuta, kiwanja kidogo cha ndege, Taka)
- Mabwawa ya maji, barabara, mashimo kwa ajiri ya kuchimba udonga utakaotumika wakati wa ujezi.
3. Ujenzi wa Kituo cha majini na gati
Mafuta ghafi, yanayosafirishwa kupitia bomba yatahifadhiwa kwenye kituo kilichopo Chongoleani kwenye mwambao wa Tanga, kabla ya kusafirishwa na kuuzwa kwenye nchi nyingine. Meli zitapakia mafuta ghafi kwenye kituo kilichopo maji yenye kina kirefu.