Utaratibu huu wa malalamiko unaeleza nini cha kufanya ikiwa una malalamiko kuhusu shughuli zinazohusiana na mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki au shughuli za waikandarasi watakao kuwa wanafanya kazi kwenye mradi.
Tunafanya nini tunapopokea malalamiko yako?
Mtu binafsi, chama, jumuiya, au taasisi inaweza kutoa taarifa ya malalamiko kuhusiana na timu za wafanyakazi wa mradi wa EACOP au shughuli za wakandarasi wao kwa kufuata utaratibu ufuatao;
Ikiwa unaamini kuwa mradi wa EACOP unawajibika kwa hali isiyofaa, unaweza toa taarifa ya malalamiko kupitia Afisa wa Uhusiano wa Jamii au wafanyakazi wengine wa mradi.
HATUA ZA KUFUATA KWENYE KUFANYIA KAZI LALAMIKO/MALALAMIKO YAKO
Hatua ya kwanza
- Kama malalamiko yanaweza kufanyiwa kazi mara moja, afisa mahusiamo atachukua hatua ili kushughulikia suala hilo moja kwa moja.
- Mara baada ya hatua ya kurekebisha kuchukuliwa, utasaini Fomu ya Kukubaliana na Kufungwa kwa malalamiko kwa usaidizi wa afisa mahusiamo na utapewa nakala.
- Unaweza kuomba mtu ashuhudie mchakato wa lalamiko/malalamiko yako
Hatua ya Pili
- Ikiwa malalamiko hayawezi kutatuliwa mara moja, utajaza fomu ya malalamiko na kusubiri barua ya kupokelewa ndani ya siku 7.
- Uchunguzi utafanyika kuhusu malalamiko yako ndani ya siku 15 ili kujua kama kuna madhara yaliyosababishwa na mradi wa EACOP
- Suluhisho litapendekezwa na kutekelezwa, ikiwa unakubaliana.
Utasaini Fomu ya Kukubaliana na Kufungwa kwa malalamiko na utapewa nakala.
Zingatia: Ikiwa kwenye uchunguzi itabainika kuwa Malalamiko hayana msingi, utapokea barua inayoelezea kwa nini malalamiko yalikataliwa
NGAZIZA RUFAA
Rufaa ya Kwanza
- Ikiwa hujakubaliana na ufumbuzi uliopendekezwa ndani ya mwezi mmoja, Kamati ya Usimamizi wa Malalamiko itakutana
- Kamati itajumuisha wafanyakazi wa mradi, na wawakilishi wa serikali au watu wengine. Kamati itachunguza malalamiko na sababu za kukataa kwako na kutafuta suluhisho lingine linalofaa.
- Ikiwa unakubaliana, utasaini Fomu ya Kukubaliana na Kufungwa kwa malalamiko.
Rufaa ya Pili
- Kama hukubaliani na suluhisho lililopendekezwa na kamati, malalamiko yako yatatumwa kwa Kamati ya Rufaa ambayo itafikiria kupendekeza suluhisho lingine.
- Ikiwa unakubaliana suluhisho, utasaini Fomu ya Kukubaliana na Kufunga kwa malalamiko.
- Kama hukubaliani na suluhisho, malalamiko yatafungwa na utapata barua ya kufungwa kwa malalamiko kutoka kwa mradi.
- Malalamiko yatapewa kwa Idara ya Sheria ya Mradi. Mara suluhisho linapopatikana na unapakubaliana na, hatua ya kurekebisha itatekelezwa. Utaombwa kusaini kipengele cha kufungwa kwa malalamiko katika fomu ya malalamiko ili kufunga shauri. Fomu ya Kukubaliana na Kufungwa kwa malalamiko itajazwa na utapewa nakala.
KUMBUKA
Mara moja suluhisho linapopatikana na unapokubaliana nalo, hatua ya kurekebisha itatekelezwa. Utaombwa kusaini kipengele cha kufungwa kwa malalamiko katika fomu ya malalamiko ili kufunga shauri.
Fomu ya Kukubaliana na Kufungwa kwa malalamiko itajazwa na utapewa nakala.
Afisa Uhusiano wa Jamii atakuwa mtu wa kuwasiliana naye wakati wa mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa malalamiko. Hata hivyo, tafadhali zingatia kwamba hana mamlaka ya kufanya uamuzi wowote kwa niaba ya kampuni.
Utoaji wa taarifa na mchakato mzima wa kutatua suluhisho ni bure na hauhitaji fedha kutoka kwa mlalamikaji