Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki utasaidia shughuli za kijamii kwenye eneo litakapopita.
Wafanyakazi wa Mradi sasa wanafanyia kazi mkakati wa shughuli za kijamii (CSR), kutambua mahitaji na kuelewa kuhusu mipango ya maendeleo ya wilaya iliyopo, inayohusiana na shughuli zinazoendelea na wadau. Awamu hii ni muhimu ili kuhakikisha usahihi wa shughuli zetu za baadaye za kijamii.
Miradi ambayo tutaifadhili kwa siku za usoni itaandaliwa kwa misingi ya kuwashirikisha wadau mbalimbali, jamii, serikali za mitaa na wadau wote wanaohusika kwenye ufadhili.
Miradi yote ya kusaidia jamii itatengenezwa kwa kuzingatia taratibu ambazo ni endelevu. Hii itahusisha wadau hasa wanufaikaji katika hatua zote za kutengeneza miradi.
Pia utaratibu wetu wa kufadhili miradi utakuwa wa wazi mda wote.: Tutahakikisha miradi itakayofadhiliwa chini ya EACOP inaendelea kuwepo hata baada ya ukomo wa ufadhili.
Tutachangia miradi ya kijamii kadri iwezekanavyo kusaidia na tutaendelea kusaidia lakini hatutazuia mamlaka za mitaa au taifa katika jitihada zao za kutekeleza majukumu yao ya kikatiba.