Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki ni bomba la mafuta yanayosafirishwa nje nchi lenye urefu wa kilometa 1,445 ambalo litafirisha mafuta ghafi ya Uganda kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga nchini Tanzania
Kutokana na hali ya mafuta ya Uganda, bomba litatakiwa kuwa na joto kutoka mwanzo hadi mwisho, na kulifanya EACOP kuwa bomba refu zaidi duniani lenye joto
Serikali za Uganda na Tanzania zimetia saini Mkataba baina yao (IGA) kwa ajili ya Mradi wa bomba. Kusainiwa kwa mkataba ni hatua muhimu sana ambayo inaweka msingi wa mradi huo pamoja na mikataba mingine ya mradi, ikiwa ni pamoja na Mikataba ya Serikali ya Nchi Mwenyeji, Mikataba ya Wadau na Mikataba ya Ufadhili. Mkataba huu unaonyesha uamuzi wa nchi hizi mbili kuanza ujenzi wa bomba la mafuta. Utekelezaji wa mradi wa EACOP umeanza tayari kwa tafiti mbalimbali za kiufundi, kimazingira na kijamii nchini Uganda na Tanzania. Utafiti wa Mwisho wa Kiuhandisi (FEED), pamoja na Tathmini ya Athari za kimazingira na kijamii, na Tafiti za Miamba sasa zinafanyika katika nchi zote mbili.
Utafiti wa wa Mwisho wa Kiuhandisi (FEED), ni utafiti wa msingi wa kiuhandisi unaofanywa kwa undani ili kupata taarifa za kiufundi za mradi. Ni shughuli ya kiuhandisi ambayo inahakikisha mpango kamili wa mradi kabla ya kuwasilisha zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. FEED itaandaa taarifa za msingi za kiuhandisi za mradi wa EACOP ambazo ztakuwa msingi wa Uhandisi wa kina, Uamuzi wa Mwisho wa Uwekezaji, umepangwa kumalizika Desemba 2017, na kupelekea kuanza utekelezaji wa mradi na awamu ya ujenzi wa bomba. Shughuli za FEED zitahusisha kupungua kwa upana wa njia ya bomba kutoka kilometa 2 hadi mita 30 kwa kutumia data za kiufundi, kimazingira na kijamii ambazo zinakusanywa kupitia tafiti zinazoendelea. Taarifa za FEED ni pamoja na taarifa za ujenzi wa mradi, msingi wa ramani (basis of design), ramani (alignment sheet), michoro ya eneo (plot plan layouts), mpango wa utekelezaji wa mradi, ratiba, makadirio ya gharama na wito wa maandalizi ya zabuni. Shughuli za FEED zinakadiriwa kudumu kwa kipindi cha miezi 8.
Bomba litatengenezwa na Engineering Procurement and Construction Management (EPCM) mkandarasi ambaye atachaguliwa kupitia mchakato wa zabuni na kusimamiwa na Kampuni ya bomba la mafuta ambayo ni ya ubia kati ya Kampuni ya Mafuta ya Uganda, Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania na makampuni matatu ya mafuta, CNOOC, TOTAL na TULLOW
Bomba litapita nchi 2, Uganda na Tanzania. Nchini Uganda, litaanzia Hoima; kupitia wilaya 8 na wilaya 24 kwa umbali wa kilomita 296, kwenda Tanzania ambapo itavuka mikoa 8 na tarafa 24 hadi kwenye bandari ya Tanga kwa umbali wa kilomita 1,149.
Kufuatia utafiti wa kina uliofanywa na serikali za Uganda, Tanzania na Kenya. Serikali ya Uganda ilichagua njia ya Kabaale (Hoima) – Tanga kwa sababu ya kuwa na gharama ndogo zaidi, imara zaidi kwa ajili kutoa mafuta ya kwanza ya Uganda, ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.
Ujenzi wa bomba utaanza baada ya Uamuzi wa Mwisho wa Uwekezaji uliopangwa kuanza mwishoni mwa 2017 na utadumu kwa miezi 36.
Bomba litafukiwa kwa kina cha hadi mita 2. Litafukiwa chini ya zaidi katika maeneo ambayo linavuka mito au barabara. Sehemu pekee za miundombinu ya bomba ambazo zitaonekana kwa macho itakuwa vituo vya kusukumia mafuta, baadhi ya mitambo ya kupoozea joto (transformers) na vituo vya kuhifadhia na kupakia. Mara baada ya bomba kujengwa, udongo uliotolewa juu ya bomba utarejeshwa mahali pake.
Bomba litaonyeshwa kwa alama tofauti ili kuonyesha dalili ya uwepo wake, eneo la karibu, bidhaa zinazobebwa, na jina na mawasiliano ya kampuni ya kampuni inayoliendesha. Alama hizi zitasaidia umma kugundia eneo la bomba na kuzuia uchimbaji au uharibifu wowote.
Usalama ni jambo la msingi sana kwenye mradi. Bomba la Mafuta ya Mafuta la Afrika Mashariki linachukua hatua stahiki ili kuhakikisha kwamba masuala ya afya, usalama na mazingira yanafanyiwa kazi wakati wa kupanga, kujenga, na kuendesha bomba. Bomba litafukiwa- na njia imechaguliwa kwa makusudi ili kuepuka hatari ya tetemeko la ardhi, volkano, mafuriko au majanga mengine ya asili. Uhandisi utahakikisha vifaa vitakavyo chaguliwa kama mabomba ni salama sana na hayatashika kutu au kuvuja.
Mpango wa kudhibiti uvujaji wa mafuta ni sehemu ya mradi wa bomba. Mpango huo unahakikisha kwamba, katika tukio la dharura, tumejiandaa kuchukua hatua za haraka, kupitia kitengo cha teknolojia ya kudhibiti na mafunzo ya kusimamia, kupunguza na kuzuia kuvuja kwa bomba mara tu baada ya kugundua uvujajji.
Kusafirisha mafuta kwa reli au barabara ni ghali zaidi na hatari zaidi kuliko bomba. Usafiri wa mafuta yasiyosafishwa kwa njia ya barabara unahitaji magari 2,000 kila siku kwenye barabara jambo ambalo linaweza kusababisha hatari za usalama wa barabara, pamoja na mazingira na masuala ya kijamii. Kusafirisha mafuta kwa reli au barabara kunaweza kutumika kwa kiasi kidogo cha mafuta kwa umbali mfupi, hasa kama miundombinu ya reli na barabara ipo tayari. Mabomba ni salama, yana ufanisi na, kwa sababu wengi huchimbiwa chini, ni nadra sana kuonekana.
Kampuni ya Bomba la mafuta itahitaji kupata ardhi kwenye njia iliyopendekezwa ya ujenzi na uendeshaji wa bomba na miundombinu inayohusiana nayo. Kipaumbele katika kubuni na eneo la miundombinu itakuwa kuepuka kuhamishwa kwa watu. Kwa miundo mbinu ya kudumu kama barabara, pampu, vituo vya kuongezea joto na valvu za kuzuia, ardhi itapatikana kutoka kwa wamiliki wake, kwa niaba ya Serikali. Hata hivyo, sehemu kubwa ya ardhi itakodishwa na Kampuni ya Bomba wakati wa kipindi cha ujenzi na kwa ajili ya miundo mbinu ya muda mfupi, kama vile makambi na yadi.
Kampuni ya Bomba itaendesha mchakato wa upatikanaji wa ardhi kwa niaba ya serikali za Uganda na Tanzania – na mchakato utafanywa kulingana na sheria za nchi na viwango vya kimataifa
Mradi, kwa niaba ya kila Serikali, umedhamiria kutoa fidia ya haki na ya kutosha kwa ajili ya hasara kutokana na makazi na / au kiuchumi, kulingana na kanuni za kitaifa na viwango vya utendaji wa IFC. Kupitia uandaaji wa mipango ya uhamishaji makazi, malipo stahiki ya uhamishaji yatatolewa baada ya kushauriana na kaya zinazostahili. Ripoti za uthamini kutoka kwa Mthamini Mkuu Serikali, na nyaraka za RAP zitapelekwa kwa kila Serikali kwa ajili ya mapitio na uidhinishaji. Baada ya hapo Kampuni ya Bomba itawasiliana na kaya iliyoathiriwa kwa ajili ya kuandaa mikataba ya fidia ya ardhi. Mikataba yote itasainiwa na watu wanaostahiki walioathiriwa na mradi (PAPs), na fomu ya idhini ya mwenza (mke au mume), mwakilishi wa viongozi wa jamii, mwakilishi kutoka kwa mwendelezaji, na wawakilishi kutoka kwa mamlaka husika watakaobainishwa wakati wa awamu ya kupanga. Fidia itawasilishwa moja kwa moja kwa kaya iliyoathiriwa au mtu binafsi kulingana na masharti yaliyowekwa katika mikataba. Kwa mujibu wa kanuni za kitaifa, fidia itatolewa kabla ya upatikanaji na uchukuaji wa ardhi.
EACOP lina faida kwa Uganda na Tanzania ambayo inajumuisha utengenezaji wa nafasi za kazi, bidhaa/huduma za ndani (local content), miundombinu mpya, vifaa, uhamishaji wa teknolojia na uimarishaji wa ukanda wa kati (central corridor) wa Uganda na Tanzania. Faida muhimu ya moja kwa moja ambayo itatoka kwenye bomba la mafuta itakuwa kuongezeka kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kwa serikali zote mbili. Bidhaa/huduma za ndani ni jambo la muhimu kwa washiriki wa mradi wa EACOP na litaunganishwa kikamilifu katika mkakati wa mkataba pamoja na mipango ya mafunzo. Mpango wa bidhaa/huduma za ndani unaandaliwa ili kuongoza mchakato wa utekelezaji.
Inatarajiwa kwamba Bomba litatoa mafunzo kwa watu wanaohusika katika utekelezaji wake, kutoka kwa mafundi wa kuchomea hadi kwa wafanyakazi wa uendeshaji wa bomba, ambao kwa kiasi kikubwa watajumuisha wananchi, wanaopatikana karibu ya eneo la mradi huo. Kwa kufanya hivyo, ongezeko hili katika uwezo wao litafaidisha makundi haya kwa muda mrefu kwa kuwa wataweza kufanya kazi kwenye miradi kama hiyo au viwanda vingine kwa siku za baadaye.
Watu wapatao 10,000 wataajiriwa wakati wa ujenzi na uendeshaji wa mradi huo. Mradi wa EACOP umeazimia kuimarisha matumizi ya wafanyakazi na makandarasi wa ndani kupitia mipango ya mafunzo na msaada kwa makampuni ya ndani kwa kuimarisha ujuzi na uwezo wao, kutengeneza ajira moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kusaidia bidhaa/huduma za ndani na manunuzi. Bomba litajenga ujuzi wa muda mfupi (miaka 2-3) ambao unaweza kutumika katika mradi mwingine wa miundombinu / usafirishaji nje. Inatarajiwa kwamba wafanyakazi wa kawaida ambao watashiriki katika awamu ya ujenzi ya mradi uliopendekezwa watatafutwa kutoka ndani ya nchi, karibu na eneo la mradi, ambapo itaendeleza zaidi uwezo wa ndani
- Mradi wa EACOP utahakikisha kuwa masuala ya afya, usalama, kijamii, kiuchumi na kimazingira yanashughulikiwa katika awamu ya kupanga, ujenzi na uendeshaji wa bomba. Njia ya bomba imechaguliwa ili kuepuka maeneo muhimu ya kimazingira kama vile mbuga za wanyama na maeneo yenye idadi kubwa ya watu. Vituo vitawekwa na kuendeshwa kwa umakini ili kupunguza athari yoyote ya kimazingira na ya kiikolojia.Tumeandaa mkataba wa bioanuai ambao unaweka kanuni za kazi yetu. Kwa mujibu wa mkataba huu, tunafanya shughuli zote za EACOP wakati:Tunaepuka athari isiyo ya lazima kwa mazingira, bioanuai na jamii husika.Tunapunguza athari yoyote isiyoweza kuepuka kwa mazingira, bioanuai na jamii husika.Tunarudisha katika hali ya awali maeneo yaliyoathirika na kusimamia urejeshwaji wake.Tunaondoa athari yoyote ya mabaki ili kupata faida
Tunajitahidi kuzuia tukio la hitilafu kwenye bomba, lakini katika tukio la dharura ya bomba, tumejiandaa kuchukua hatua za haraka. Mpango wa dharura wa kudhibiti uvujaji wa mafuta ni sehemu ya mradi wa bomba pamoja na teknolojia kudhibiti, kupunguza na kuzuia uvujaji wa bomba mara tu unapogunduliwa. Mazoezi ya mara kwa mara na wafanyakazi wa ndani wa dharura, kama vile idara za zimamoto na polisi, pia kuhakikisha mwitikio wetu kwenye tukio unaratibiwa vizuri na wenye ufanisi. Mafuta mazito katika bomba yanapaswa kuwa na joto la 50 °C ili mafuta yaweze kutiririka kwenye bomba, hiyo inamaanisha kwamba ikiwa kuna uvujaji, mafuta yataganda kwa haraka sana, na kupunguza athari kwenye ardhi. Katika hali ya uchafuzi, hatua zitachukuliwa ili kurejesha ardhi kwa hali yake kabla ya tukio hilo.
Mradi wa EACOP umedhamiria kuhakikisha ushiriki kikamilifu wa wadau wake wote kwa mujibu wa kanuni za ushiriki, kuheshimu haki za binadamu, kutokuwa na ubaguzi, uwezeshaji, uwazi na uwajibikaji. Kwa hivyo ushiriki wa wadau utakuwa kwa ajili ya; kuanzisha mahusiano ya kudumu na wadau, kutoa maelezo ya mradi ili kuwawezesha wadau kushiriki kikamilifu wakati wote wa mchakato, kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau kuelewa wasiwasi wao na kutafuta ufumbuzi, kujitolea kushughulikia matatizo ya wadau kwa njia ya haki na yenye ufanisi na kushiriki kikamilifu kwenye majadiliano ya wazi kwa wadau mbalimbali. Maafisa wa Uhusiano wa Jamii (CLO) hufuatilia athari za Mradi wa EACOP kwenye jamii na asasi za kiraia, viongozi wa serikali za mitaa na wadau wa utalii. Hii inajumuisha kusimamia uendeshaji wa tafiti za msingi na tathmini ya athari za kijamii, na usimamizi wa mipango ya athari za kijamii ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi – upatikanaji wa ardhi na uhamisho wa makazi, kushughulikia malalamiko, ajira za ndani, na ushiriki wa wadau.
Mara mafuta kutoka Ziwa Albert yatakapokuwa yamepungua, (karibu miongo 3 kutoka sasa), inawezekana kwamba uvumbuzi mwingine wa mafuta unaweza kufanywa nchini Uganda au katika nchi zinazozunguka kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Tanzania na Sudan Kusini. Muda halisi wa matumizi ya bomba ni mrefu zaidi kuliko yale yaliyotakiwa kwa mauzo ya mafuta ghafi ya Ziwa Albert. Kwa ujumla wakati mabomba yamejengwa (na kulipiwa), ni rahisi sana kwa mafuta mengine ghafi kuzalishwa na kusafirishwa kwa njia ya bomba – hivyo hata baadhi ya visima vidogo zaidi vya mafuta vinaweza kuwa na faida za kiuchumi. Mara baada ya pande zote husika kuamua kwamba bomba halihitajiki, basi awamu ya kuacha kutumiwa itaanza. Kwa kuwa bomba lipo ardhini, linaweza kusababisha athari ndogo ya mazingira lisafishwa na kuliacha ardhini. Hiyo itapaswa kufanyiwa uchunguzi wa mazingira na kuidhinishwa serikali.
Mafuta yanayosafirishwa na mabomba yanakuwa hayajasafishwa hivyo hayafai kwa matumizi yakiwa katika hali hiyo. Kwa kuwa mafuta hayo ni mazito hayawezi kutumika kwa kupikia au matumizi mengine. Kuna mkakati wa kujenga kituo cha kusafishia mafuta ambayo yanakidhi mahitaji ya mafuta ya petroli ya Uganda na maeneo ya majirani, na kiasi kinachobaki kisafirishwe nje kupitia bandari ya Tanga nchiniTanzania.
Bei hutegemea gharama za mradi miongoni mwa mambo mengine muhimu. Bei ya mwisho itajulikana baada ya kukamilika kwa FEED na kutolewa kwa mkataba wa ujenzi kwa mkandarasi Engineering Procurement and Construction Management (EPcm). Imekubaliwa kuwa bei haipaswi kuwa zaidi ya dola 12.2 kwa pipa.
Bomba litakuwa linamilikiwa na wanahisa wa mradi huo, yaani; Serikali ya Jamhuri ya Uganda (Kampuni ya Mafuta ya Uganda) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Shirika la Maendeleo la Petroli), na makampuni matatu ya mafuta CNOOC, TOTAL na TULLOW PLC, ambayo kwa pamoja yatakuwa yanasafirisha mafuta kwenda nje. Kampuni huru ya Bomba la Mafuta itaanzishwa, na itaingia katika mikataba na makubaliano kadhaa: na serikali mwenyeji wa eneo ambalo bomba litapita, na makandarasi wa kujenga bomba na miundo mbinu yote muhimu. Kampuni ya Bomba la Mafuta itakuwa mmiliki wa miundo mbinu ya bomba; hata hivyo haitamiliki mafuta ambayo yatakuwa yanapita kwenye miundo mbinu yake. Kampuni ya Bomba la Mafuta itaendesha bomba na itakuwa na jukumu la usalama wa kudumu na kutoingiliwa kwa shughuli za bomba.
Makadirio ya jumla ya gharama za uwekezaji wa mradi huo ni $ 3.5 bilioni. Mtaji wa dola bilioni 3.5 unaohusishwa na ujenzi na uendeshaji wa bomba utaingizwa moja kwa moja katika uchumi wa Tanzania na Uganda, na kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) kwa zaidi ya 60% wakati wa awamu ya ujenzi
Benki na taasisi za kifedha zitatoa sehemu kubwa ya mtaji wa $ 3.5 bilioni kwa mradi wa EACOP. 70% ni kiwango cha madeni yanayotegemewa kwa ajili ya mradi huo. 30% iliyobaki itafadhiliwa na wadau wa mradi ikiwa ni pamoja na Serikali za Uganda, Tanzania na washirika; Total, Tullow Pty Ltd na CNOOC