skip to Main Content

Taarifa Ya Mradi – 16 Septemba 2021

Mafuta yanayozalishwa nchini Uganda katika eneo la ziwa la Lake Albert yatasafirishwa nchini Tanzania kupitia Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) na katika pwani ya bandari ya Tanga na mafuta hayo yatauzwa katika soko la dunia. Uzalishaji wa mafuta hayo unatarajia kuanza mwaka 2025. Muundo wa kisheria na kibiashara wa EACOP ulianzishwa katika Mkataba wa nchi hodhi uliosainiwa katika miezi ya Aprili 11, 2021 na Mei 20, 2021 kati ya EACOP na Serikali za Uganda na Tanzania mtawalia. Aidha, mikataba ya nchi hodhi iliweka msingi wa mahusiano kati ya EACOP na nchi hodhi katika masuala ya ardhi, afya, kijamii, usalama, viwango, haki za binadamu, fursa kwa wazawa, usimamizi wa fedha, uidhinishaji na usuluhishaji wa migogoro.

Nchini Uganda, EACOP kimsingi inasimamiwa na Mamlaka ya Petroli ya Uganda pamoja na Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira. Nchini Tanzania, EACOP inasimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Pamoja Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). Nchini Uganda, mfumo wa EACOP una kilomita 296 za bomba litakalojengwa na vituo viwili (2) vya kusukuma mafuta. Nchini Tanzania, mfumo wa EACOP una kilometa nyingine 1,147 za bomba, kituo cha kuhifadhi mafuta, vituo vinne (4) vya kusukuma mafuta na vituo viwili (2) vya kupunguza mgandamizo wa mafuta. Bomba linahitaji mkuza wenye upana wa mita 30, sawa sawa na miradi mingine inayotumia muundo wa mstari kama barabara, reli au njia za umeme. Ni muhimu kutambua kuwa bomba liliotengenezwa ili liweze kutunza joto litawekwa katika mtaro na litafukiwa chini ya ardhi baada ya ujenzi wake kukamilika aidha, udongo wa juu na uoto utarudishwa katika hali yake ya asili na ardhi itakuwa wazi kutumika na watu pamoja na wanyama.

Uendeshaji wa Mradi ukianza, mfumo wa EACOP utafuatiliwa kwa mkongo maalum, wenye uwezo wa kutambua mabadiliko ya joto pamoja na mitetemo katika urefu wote wa bomba. Pia, kutakuwa na mfumo kabambe wa teknolojia ya kutambua uvujaji utakaokua na koki kuu za kufunga na kuzuia uvujaji kwa lengo la kuhakikisha uzuiaji wa uvujaji na/au umwagikaji wa mafuta. Mkuza wa bomba umesanifiwa kuhakikisha unapunguza madhara ya kimazingira na kijamii. Kutokana na muundo wa mstari wa bomba, sehemu kubwa ya madhara ni ya kiuchumi, madhara ya uhamishaji watu katika maeneo yao ya asili au madhara ya kiuchumi. Mradi utawafidia au kuwarudisha katika hali zao jamii zilizoguswa kwa kuzingatia Makubaliano ya Equator na Viwango vya Kiutendaji vya Kampuni ya Kimataifa ya Kukopesha fedha (IFC), na sheria za Uganda na Tanzania. Hata hivyo, kwa baadhi ya Waguswa waliopata madhara ya utwaaji wa makazi na mashamba ya kibiashara, fidia yao imezingatia sheria za Tanzania na Uganda pamoja na Viwango vya Utendaji vya IFC.

Nchini Tanzania, kuna Waguswa wa Mradi (PAPs) 9,513 (idadi kubwa ni Waguswa wa makazi/kaya lakini pia taasisi za kibiashara na zile za serikali). Kati yao, Waguswa 331 (3.5%) wamehamishwa makazi na wamepewa chaguzi kati ya nyumba mbadala (za kiwango kikubwa kuliko walizokuwa wakiishi/wanazoishi) au fedha taslimu. Idadi kubwa ya Waguswa waliohamishwa makazi wamechagua nyumba mbadala na ujenzi wa nyumba hizi unaendelea. Nchini Uganda kuna Waguswa wa Mradi 3,648. Kati yao, 203 (5.5%) wamehamishwa makazi na idadi kubwa wamechagua nyumba mbadala ambazo ujenzi wake unaendelea. Kati ya kanuni za msingi za kulipa fidia ni pamoja na kumheshimu kila mguswa na kumlipa thamani kamili ya fidia yake. Kila Mguswa atasaini mkataba binafsi wa fidia (kwa sasa mchakato huu unaendelea na hadi kufikia Septemba 2022, Waguswa 4,612 kati ya 9,513 nchini Tanzania na 2,622 kati ya 3,648 nchini Uganda wamesaini mikataba yao ya fidia. Hakuna ardhi itakayotumiwa na Mradi mpaka fidia iwe imelipwa na notisi ya kuhama iwe imesainiwa na kutolewa.

Waguswa wanaostahiki pia watakuwa na stahiki ya kapu la mpito kuwapatia chakula katika kipindi hicho na watajumuishwa katika mpango wa kurejesha mbinu za kupata mahitaji. Mchakato wa utwaaji ardhi unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2023. EACOP, wabia wake na Serikali mbili hodhi zitahakikisha kuwa Mradi unatekelezwa kwa mfano wa kuigwa kwa kuzingatia uwazi, Mafanikio kwa wote, Maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na maendeleo endelevu kwa Mazingira na kuheshimu Haki za Binadamu.

Back To Top