Deprecated: Array and string offset access syntax with curly braces is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-includes/script-loader.php on line 706

Deprecated: Array and string offset access syntax with curly braces is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-includes/script-loader.php on line 706

Deprecated: Array and string offset access syntax with curly braces is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-includes/script-loader.php on line 707

Deprecated: Array and string offset access syntax with curly braces is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-includes/script-loader.php on line 707

Deprecated: Function create_function() is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-content/plugins/masterslider/includes/classes/class-msp-main-widget.php on line 95

Deprecated: Array and string offset access syntax with curly braces is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-content/plugins/si-contact-form/captcha/securimage.php on line 727

Deprecated: Array and string offset access syntax with curly braces is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-content/plugins/Ultimate_VC_Addons/admin/admin.php on line 715

Deprecated: Function get_magic_quotes_gpc() is deprecated in /home/eacop/public_html/SW/wp-includes/load.php on line 760
Uncategorized – EACOP

Uncategorized

Marais Museveni na Magufuli waweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi

Marais Museveni na Magufuli waweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi

Rais Yoweri Museveni na mwenzake wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli leo wamezindua ujenzi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki kutoka wilaya ya Hoima, nchini Uganda hadi bandari ya Tanga, nchiniTanzania.

Viongozi hao wawili walitumia fursa hiyo kuthibitisha umuhimu wa utangamano wa haraka wa jumuiya ya Afrika Mashariki ili kurahisha mipango ya pamoja, ufadhili na utekelezaji wa miradi mikubwa ambayo ni muhimu kwa maendeleo na mabadiliko ya ukanda huu.

Bomba la mafuta lenye joto, ambao ni refu zaidi duniani, litagharimu dola bilioni 3.5 na ujenzi wake utakamilika mwaka 2020 ambapo Uganda itajiunga na kundi la nchi zinazozalisha mafuta. Ujenzi wa bomba la mafuta utafanywa na Total E&P, CNOOC na Tullow Oil pamoja na serikali mbili za Uganda na Tanzania. Bomba la mafuta litakapomilika litasafirisha mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa kila siku.

Akizungumza wakati wa sherehe Rais Museveni alimshukuru sana Rais Joseph Pombe Magufuli, serikali ya Tanzania na Watanzania kwa makubaliano mbali mbali na serikali ya Uganda na wabia ambayo yameharakisha mradi huu.

Alisema kwa sababu ya makubaliano mbali mbali na serikali ya Tanzania, gharama ya kusafirisha pipa la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga itakuwa dola 12.2 kwa pipa, na kuyafanya mafuta ya ghafi ya Uganda kuwa na faida hata kwa kiwango cha leo cha dola 50 kwa pipa.

“Kwa niaba ya wananchi wa Uganda ninawashukuru Rais Magufuli na ndugu zetu wa Tanzania kwa makubaliano mbali mbali yanayohusiana na bomba la mafuta. Hakutakuwa na ushuru wa kupitisha mafuta, hakutakuwa na kodi ya ongezeko la thamani, hakutakuwa na kodi ya mapato ya kampuni, wametupa msamaha wa kodi kwa miaka 20, wametupa eneo la bure ambako bomba la mafuta lipita na kuahidi kununua hisa katika bomba la mafuta” alisema Rais Museveni

Rais aliyaomba mataifa yote ya Afrika Mashariki kulichukulia bomba la mafuta la Afrika Mashariki kama mali ya Afrika Mashariki, akibainisha kuwa kwa kugundulika kwa mafuta na gesi katika nchi nyingine katika eneo hilo, bomba litakuwa chombo cha kusafirishia mafuta kuelekea baharini kutoka nchi zote za Afrika Mashariki.

Rais Museveni aliwapongeza wabia katika mradi wa bomba la mafuta (Total, CNOOC na Tullow) na akawahakikishia kuwa kwa na uhusiano mzuri wa kikazi, kila mmoja atafaidika.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimshukuru Rais Museveni na serikali yake kwa kuiamini Tanzania na kuchagua njia ya Tanga kwa mradi licha ya fursa nyingine zilizopo.

Alisema kwa mafuta kuja Tanga, Tanzania sasa itanunua mafuta ghafi kutoka Uganda badala ya kuingia gharama kubwa za kuagiza kutoka nchi za Kiarabu, huku akionyesha kuwa Uganda pia itaiuzia mafutaTanzania kwa gharama nafuu.

Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Tanzania pia itapata ujuzi na utaalamu kutoka kwa wataalamu wa Uganda ambao watakuwa na uzoefu katika sekta ya uchimbaji mafuta.

Aliwahimiza makandarasi ili kuhakikisha kuwa wanakamilisha mradi kwa muda unaotakiwa, akisema kitu chochote kinyume cha hapo kitaleta sifa mbaya kwao na kwa nchi zao.

Read more...

Serikali za Uganda na Tanzania zasaini Mkataba wa Bomba la Mafuta

Serikali za Uganda na Tanzania leo zimetia saini Mkataba, wa  Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Kusainiwa kwa mkataba huu ni hatua muhimu sana kwa Mradi wa EACOP. Unaweka msingi wa mradi huo pamoja na mikataba mingine ya mradi, ikiwa ni pamoja na Mikataba ya Serikali ya Nchi Mwenyeji, Mikataba ya Wabia na Mikataba ya Ufadhili, ambayo sasa itajadiliwa. Mkataba huu unaonyesha uamuzi wa Jamhuri ya Uganda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuanza ujenzi wa bomba la mafuta lenye joto ambalo ni refu zaidi duniani, kwa manufaa ya nchi zote mbili na makampuni ya mafuta lakini pia kwa manufaa ya eneo lote  la Afrika Mashariki.

Pia, ni hatua muhimu kwa maendeleo ya Tilenga (mradi wa mafuta wa kaskazini mwa Ziwa Albert) na Miradi mingine ya mafuta ya Kingfisher kwa kuwa bomba la mafuta ni moja ya njia muhimu za kufikia soko kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano (MoU) wa uuzaji wa rasilimali za mafuta na gesi za Ziwa Albert uliosainiwa mwaka 2014 kati ya Serikali ya Uganda na Ushirika wa Makampuni ya Mafuta.

Ushirika wa Makampuni ya Mafuta, CNOOC, Total na Tullow Uganda Operations Pty Ltd zinachukua fursa hii kuzipongeza na kuzishukuru Serikali za Uganda na Tanzania kwa kufikia kwa haraka hatua hii ya kusaini mkataba huu na kwa mchango wao endelevu kwenye utekelezaji wa mradi huu

Washirika wa JV wamedhamiria kikamilifu na wana hamasa ya kutosha ili kufikia lengo la mauzo ya mafuta ya kwanza yaliyopangwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2020 kwa kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali zote mbili ili kuhakikisha kuwa mradi wa EACOP unaendelea zaidi (hususani kukamilisha Mradi wa Mwisho wa Uhandisi, tathmini ya athari ya kimazingira na kijamii na Utafiti wa mwisho wa kiuhandisi wa miamba, udongo na maji) pamoja na maendeleo ya utafutaji mafuta huko Tilenga na Kingfisher.

Read more...